PALLASO ambay ni ndugu wa msanii wa muziki  nchini Uganda, Jose Chameleone, ameshambuliwa na kuumizwa nchini Afrika Kusini  katika shambulio lililodaiwa kuwa ni sehemu ya machafuko yanayoendelea dhidi ya wageni nchini humo (Xenophobia).

 

Akiwa ndani ya gari katika hatua zake za ku-shoot video nchini humo katika mji wa Durban, inadaiwa alivamiwa na watu na kushambuliwa ikiwa pamoja na kuchomwa kisu.

 

Naye Chameleone akizungumzia tukio hilo kupitia mtandao na ukurasa wake wa Twitter alitoa taarifa kuwa ndugu yake maisha yake yako hatarini.

 


Muda mfupi baada ya kushambuliwa Pallaso alituma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook akiwataka watu kumuombea kwani amefanikiwa kuwaponyoka waliokuwa wakimshambulia na alikuwa anatafuta namna ya kupata matibabu kisha arejee nchini kwake (Uganda) salama.