KILA kukicha hali ya staa wa Bongo Muvi inazidi kubadilika kutokana na kuzidi kukondeana jambo ambalo linazidi kuwashtua wengi na kubaki wakisema kwa kumuhurumia; maskini Wema. Picha ya Wema akiwa na wenzake ilisambaa kwenye kurasa mbalimbali za mtandao wa Instagram na kuwashangaza wengi kutokana na kuzidi kukonda huku wengi wakimsihi ajaribu kurudi katika hali yake ile ya zamani ya unene maana akiendelea hivyo hali itakuwa tete zaidi.

“Madam jamani… kwani hawawezi kumrudishia kipande chake cha utumbo… this is toooooooo much… mambo ya kusikiliza watu haya… hapanaaaaa maana bila kumsimanga kunenepeana asingefikia hapo alipo… Duh,” aliandika mmoja wa wadau chini ya picha hiyo.