Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akisalimiana na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(sasa Balozi mteule) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Uwesu Ngarama.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akifanya mahojiano maalum na wanahabari baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akipokea salaam ya heshima toka katika Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima leo katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020(Picha zote na Jeshi la Magereza)