Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula (kulia) akiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wakielekea kwenye kikao cha ndani kabla ya kwenda kuzungumza na wajumbe wa halmashauri kuu, na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip Mangula amewaonya wagombea wa viti vya udiwani na ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuwa wale ambao wataanza kampeni mapema kabla ya muda muafaka pamoja na kutoa zawadi mbalimbali watakatwa majina yao.

Mangula amebainisha hayo leo Februari 16,2020 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu, na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kina kanuni na taratibu zake hivyo wagombea wote wanapaswa kufuata kanuni na maadili ya chama.

Ametoa onyo kwa wagombea wote ambao wana nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuwa wale ambao wataanza kampeni kabla ya muda hawatasita kukata majina yao.


“Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, tunataka taratibu, kanuni na ya chama zifuatwe kwenye kugombea nafasi za udiwani na ubunge, wale ambao wataanza kampeni kabla ya muda pamoja na kutoa zawadi tutafyeka majina yao, bali msubiri muda ukifika ndipo muanze kujinadi,” amesema Mangula.


“Tunataka nidhamu ndani ya chama, na hakuna jamii ambayo haina taratibu namna ya kuishi, hivyo kamati za siasa chungeni sana wagombea ambao wataanza kufanya kampeni kabla ya muda wachukulieni hatua, na mkishindwa sisi tutaiwajibisha kamati nzima,”ameongeza.


Pia amewataka wana CCM kuendelea kushikamana na kuwa wa umoja hasa kwenye kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, ili chama kipate ushindi wa kishindo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amemuhakikishia Mangula kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuelekea kwenye uchaguzi, ambapo hakuna hata kiti kimoja ambacho watakipoteza, kuanzia nafasi ya udiwani na ubunge, huku akiahidi kutekeleza maagizo ambayo ameyatoa ikiwamo wagombea kuanza kampeni kabla ya muda.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, amemuomba Mangula kupeleka salamu za pongezi kwa Rais John Magufuli, kutokana na kazi kubwa ambayo anaifanya, huku akibainisha namna alivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya Miaka Mitano, kwa kufanya shughuli za kijamii kwa asilimia 80 ikiwamo sekta ya afya na elimu.

Pia amemuomba kwenda kulisemea tatizo la kutokamilishwa kwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, ambapo mwaka 2018 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofanya ziara mkoani Shinyanya alitoa ahadi ya kukamilisha hospitali hiyo, ambapo mwaka 2019 ingeanza kutoa huduma lakini hadi leo hakuna kinachoendelea huku majengo yakikaliwa na popo.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Capinduzi CCM Tanzania bara Philip Mangula, akisoma kanuni za chama leo Jumapili Februari 16,2020 wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga. Alionya wagombea kuanza kampeni mapema kabla ya muda muafaka na atakaye kiuka atakatwa jina lake.

Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Tanzania bara Philip Mangula, akiwataka wajumbe kuwa kitu kimoja hasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu  2020 ili chama kipate ushindi wa kishindo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula na kumuahidi ushindi wa kishindo uchaguzi mkuu na hakutakuwa na kiti hata kimoja kwenda upinzani iwe udiwani na ubunge.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa salamu za Serikali kwenye mkutano huo.

Mbunge wa viti maalum mkoa  Shinyanga Azza Hilal Hamad akiElezea namna alivyotekeleza Ilani ya Uchaguzi kwenye majimbo yote sita ya mkoa wa Shinyanga ikiwamo sekta ya afya na elimu.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akielezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akielezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, akielezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akielezea utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (wa kwanza kushoto), akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba katikati kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum (mwenye kofia) akiwa na wajumbe wengine kwenye mkutano wa makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula akisalimiana na wajumbe mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kufanya mkutano, akisalimiana na mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum.


Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philipo Mangula, akisalimiana na mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakar Mukadam.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara PhilipoMangula, akisalimiana na mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge.

Wajumbe wakitoa burudani kwenye mkutano huo, kwa kucheza nyimbo za CCM. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.