Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara amewajia juu watu wanaosema klabu hiyo hivi sasa inacheza vizuri akisema hakuna timu yenye uwezo wa kucheza vizuri wakati wote.

Haji ambaye anawasema Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (Simba) amesema watu hao wanaongopea umma kuwa Simba hivi sasa inacheza vizuri baada ya wao kukosoa.

Amesema simba ina wachezaji wenye viwango vikubwa na inajua inachokitaka lakini haiwezi kucheza kwa ubora muda wote lakini inapocheza vizuri sio kwasababu ya mchambuzi fulani wa soka.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL

“Kwanini asikosoe gongo wazi nayo icheze kibingwa, Narudia tena Simba haichezewi mimi nikiwepo, subirini nife au nisiwepo pale ndo mlete maneno yenu ya hovyohovyo. Nichezeeni mimi lakini sio Simba yangu,” amesema.