Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na kauli ya mwanadada Wema Sepetu na kumtaka kumuongelee vizuri mwanaye marehemu Steven Kanumba na amemtaka kukutana ili kufanya ibada ili kuondoa laana aliyopewa.

Hayo yametokea baada siku chache kupita baada ya Wema kupitia interview ya wemaApp kuwa alitoa mimba mbili za Kanumba na marehemu akupendezwa na tukio hilo na kumpa rahana kuwa atopata tena mtoto kwa mwanaume yoyote yule kutokana na kuua watoto wake wawili.

"Mimi sikuwahi kujua kama wema aliwahi kupata mimba ya Kanumba ila nimekuja kuzisikia baada ya kanumba kutangulia mbele za haki ila mimi kama mama naumia kwa hilo kwakuwa nilitamani kuwa na mjukuu" alisema mama Kanumba

"Nasikitika sana kwani alipokuwa anaongea hayo angenihusisha na mimi kuwa mama kuna hili ila namshauri wema aje tuongee kuhusu hili mimi ni mkristu naamini katika maombi namshauri twende kwenye maombi ili tuvunje hiyo laana yeye ni muislamu nipo tayari hata kama ni dua ya kiislam mimi nipo tayari ila kwa sisi kuna sala ya kuvunja laana aje mimi ni mama yake na kanumba" aliendelea kusema.

Pia Mama kanumba amemsii weka kuwa asikate tamaa maana bado mdogo ipo siku atapata mtoto kama anavyoitaji.