Mkuu wa mkoa Poul Makonda pamoja na mfanyabiashara Mohamed Dewji Mo wamejikuta wameguswa kumsaidia mtoto ambaye video yake imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha anaugulia maumivu makali baada ya maradhi ambayo yanamsumbua.

Video ya mtoto huyo ikimuonyesha analia kwa uchungu imekuwa ikipostiwa na mastaa wengi ikiwataka watanzania kumsaidia mtoto huyo mdogo aweze kupata matibabu .

Video hiyo ambayo imegusa hisia kali kwa kila aliyeiona ilimkuta Makonda pamja na Mo Dewji na kuguswa na uchungu wa mtoto huyo na kujitosa kugharamia matibabu yake na kutaka mawasiliano ya familia ili kuletwa Dar es Salaam kwaajili ya Matibabu.

Kupitia instagramu yake RC Makonda aliandika hivi;

"Nakosa amani naomba nimpeleke hospital huyu Mtoto,Tangu jana Usiku sijalala nilipoona clip ya Mtoto huyu. Najua maumivu ya Wazazi na zaidi Mtoto mwenye. Nimepiga hizi namba hakuna hata moja inayopatikana. Ndg zangu naombeni yoyote anaweza kunisaidia nimpate Mtoto huyu Nitamshukulu sana nahitaji kumpeleka hospital haraka sana, haijalishi yuko mkoa Gani nitamsafirisha na Kuhakikisha anapata matibabu".

Naye Mo Dewji aliandika hivi;