SHIRIKA la Geitasamo Paralegal Organization limetoa msaada wa kielimu kwa familia iliyoshindwa kuwapeleka watoto shule kutokana na hali duni ya maisha waliyokuwa nayo.

Anthony Mayunga ni msaidizi wa kisheria kutoka Wilaya ya Serengeti mkoani Mara alisema kuwa shirika la Shirika la Lengo Services Facility limekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Watanzania husasani wasioweza kumudu gharama za wanasheria kupata huduma za kisheria na kutoa msaada katika matatizo mbalimbali ikiwemo miradhi, ndoa , mimba za utoni, kutelekezwa kwa watoto, ardhi na mengine mengi.

Alisema kuwa haki ya kupata elimu inaweza kuonekana jambo dogo pale unapoipata lakini ni suala gumu kwa watoto wanaposhindwa kupata nafasi ya kusoma kama wenzao
Alisema kuwa hali hii iliwapata wanafunzi wawili Magdallena Julius (14) na mdodo wake Hellena Julius (12) pale wazazi wao waliposhindwa kuwapatia haki yao ya msingi kutokana na hali duni ya Maisha.

Alisema kuwa kilio hiki kiliwafikia wasaidizi wa kisheria wilayani Serengeti ambao waliamua kuhamasisha jamii, kupitia vyombo vya habari, kuchangia hawa watoto ili wapate haki yao ya elimu.

"Watoto hawa walihitaji sh.500,000/= kwa ajili ya mahitaji ya shule ikiwemo matengenezo ya viti, meza, michango ya mahindi, sukari, sare na vitu vingine vidogo vidogo vya msingi.

"Kufatia ushiriki wa vyombo vya habari watu wengi waliguswa na habari ya watoto hawa nakujitolea kuwasaidia. Mnamo Machi 15 mwaka 2019, Magdallena na mdogo wake, Hellena walionekana wakiwa wenye furaha, baada ya kuungana na wanafunzi wenzao wa kidato cha kwanza Serengeti Sekondari na kuanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwa walimu,' alisema.

Alisema kuwa wasamaria wema walijotokeza na kuchanga ambapo kuna waliochanga fedha taslimu na vitu mbalimbali kama sanduku la shule, sare, na taulo za kike ambavyo vilitosha kuwarudisha mabinti hao shuleni.

Shirika la Lengo Services Facility limekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha watanzania husasani wasioweza kumudu gharama za wanasheria kupata huduma mbalimbali na kufanikiwa. Kupitia kwa watoa huduma zaidi ya 3000 katika kila wilaya Tanzania Bara na Zanzibar zaidi ya watanzania millioni 5 hufikiwa na kupatiwa elimu ya kisheria na takribani kesi 75 000 zikirepotiwa kwa watoa huduma hao kila mwaka.