Msanii maarufu wa filamu Elizabeth Michael  Lulu, amemjibu shabiki ambaye amemwambia kuwa anafanana na watoto wa mrembo Hamisa Mobetto kwa kusema, labda mimba zake zinampendaga.


Lulu amemjibu hivyo baada ya shabiki huyo aitwaye Veinnah  ku-comment kwenye picha yake aliyopost katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo ameuliza kwa kuandika,

"Hivi Lulu mbona unafanana na watoto wa Hamisa Mobetto hivyo kuliko yeye mwenyewe, yani hapo Daylan mtupu, kuna zingine Fantasy kulikoni dada, kwakweli  jiangalie tu kwenye kioo ni wako kabisa" ameuliza shabiki huyo.

Muda mfupi baada ya Lulu kuiona comment hiyo amemjibu kwa kuandika "Itakuwa mimba zake zinanipendaga".