Kuna hatari kubwa kwa Vigogo wa Ligi Kuu England, klabu ya Liverpool kushindwa kutwaa kombe hilo baada ya kulisubiri kwa kipindi kirefu kufuatia uwezekano wa Serikali ya Uingereza kufutilia mbali shughuli zote za michezo na matukio nchi nzima kufuatia hofu ya janga la ugonjwa wa Virus vya Coronavirus.

Kama hilo litatokea kwa Serikali kufutilia mbali kwa matukio yote yakiwemo yale ya michezo basi ligi haitoweza kuendelea na hivyo Liverpool hatoweza kutwaa ubingwa huo ambao amekuwa akiusubiria kwa miaka 30 sasa.

Hata hivyo kuna uwezekano wa ligi hiyo kurejea baada ya miezi miwili ijayo kama serikali itachukua maamuzi hayo ya kufuta michezo na matukio mengine ili kuepusha mkusanyiko wa watu na hivyo kuwa rahisi kwa kuenea kwa Virusi vya Corona.

Kesi 19 za COVID-2019, maarufu kama Virusi vya Corona zimeripotiwa UK kwa mujibu wa BBC na vyombo vingine vya habari.

Upo uwezekano kwa Serikali kuchukua maamuzi ya kuvunja shughuli zote za michezo na mtukio ikwemo Premier League kwa muda wa miezi miwili.

Hiyo inamaana kuwa michezo yote iliyosalia hata chezwa na mpaka sasa hakuna anayejua hatma ya hilo.

Nchini Italia zaidi ya kesi 600 zimetajwa za watu waliyopata ugonjwa huo na mechi nyingi za Serie A zinachezwa pasipo mashabiki.

Imeandikwa na Hamza Fumo