Msanii wa muziki wa bongo Flave, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady JayDee amesema katika vitu ambavyo hafanyi mara kwa mara ni kuangalia Televisheni na kusikiliza redio.

JayDee aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa watu huwa wanamshangaa ndio hivyo hapendi.

Aliandika ujumbe huu “Katika vitu ambavyo huwa sifanyi mara kwa mara ni kuangalia TV na kusikiliza radio. Watu huwa  wananishangaa ila sipendi sana,”.

Baadhi ya mashabiki wake katika ukurasa huo walimuambia wana muelewa kwa kauli hiyo huku mwingine akimtolea mfano kuna mchezaji wa Mpira mzuri lakini hapendi mpira.

“Inatokea kuna mchezaji mmoja mkameruni alikuwa akicheza soka lakini hana mahaba na mpira wa miguu na hata ukimuuliza mechi gani inafuata anasema hajui. so inawezekana kabisa,” aliandika Augustinejr

Shabiki mwingine GP “Sasa kama hupendi hizo nyimbo zako kusikiliza redioni tunajipendekeza ama inakuwaje?

Msanii huyo alimjibu “Umeongea kitoto nashindwa nikujibu nini,”

Mwingine aliandika ujumbe huu “Sasa dada Jide unawaambiaje wanaokusikiliza kupitia redio na kukuona kwa Tv

Katika vitu ambavyo huwa sifanyi mara kwa mara ni kuangalia TV na kusikiliza Radio . Watu huwa wananishangaa ila sipendi sana.

— Lady JayDee (@JideJaydee) February 18, 2020