Masanii wa muziki wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz hivi karibuni alikuwa miongoni mwa waliopata maualiko wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star ambayo ilifanyika mjini Chicago Marekani kuanzia Februari 14 na kumalizika february 16 mwaka huu.

Ommy Dimpozi ameamua kuweka wazi kingereza kilivyomwangusha  na kujiona mnyonge sana hasa wakati aliofuatwa kwaajili ya kufanyiwa interview.

Kupitia akaunti yake ya instagram ameposti video akiwa kwenye fainali hizo na kuonyesha akisubiria kufanyiwa interviuw huku akiwaza lugha na kuandika hivi

"Sasa nikaambiwa natakiwa kuhojiwa baada ya @common 😩 yani jana ndo nilijua kwanini Shilole kaamua kuuza Wali Yani nilikuwa mpole kama nasubiri pepa la Necta kwanza hilo yai la bwana kipara kama ugomviii "