Waziri wa madini Doto Biteko akizindua rasmi ofisi ya kijiji cha nawenge wilaya ya ulanga mkoani morogoro ilijengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mahenge resources  ambayo ilikua inafanya utafiti wa madini ya kinywe huku akishudiwana mkuu wa wilaya ya ulanga Ngolo Malenya ,mbunge wa jimbo la ulanga Godfrey Mlinga, mkurugenzi wa kampuni black rock mining John De vries na wadau mbalimba wa maendeleo wilaya ya ulanga.
 Waziri wa madini Doto Biteko akikata utepe  mlangoni kama ishara ya ufungizi rasmi wa ofisi za vijiji na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya ya ulanga Ngolo Malenya na mbunge wa jimbo la ulanga Godfrey Mlinga.
Waziri wa madini Doto Biteko akiongea na wananchi na wadau wamaendeleo wilaya ya ulanga wakati wa kupokea ofisi tatu za vijiji vya wilaya hiyo zilizojengwa na kampuni ya mahenge resources .
 Wananchi na Wadau mbalimbali wa maendeleo wilaya ya ulanga wakimsikiliza kwa makini waziri wa madini doto biteko (hayupo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa ofisi za vijiji vya nawenge, Kisewe na Mdindo.
 Wadau waliolakwa katika hafla ya uzindizi wa ofisi wakisikiliza kwa makini waziri wa madini Doto Biteko (hayupo pichani)
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau kampuni ya Mahenge Resources wakipiga picha ya pamoja mbele ya jengo la ofisi ya kijiji cha nawenge,hii ni moja ya ofisi tatu zilizojengwa na kampuni ya Mahenge Resources.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya mahenge resource inayofanya utafiti wa upatikani wa madini ya graphate maarufu kama kinywe  wilaya ya ulanga mkoani Morogoro imekabidhi ofisi tatu za vijiji vya Nawenge, Kisewe na Mdindo zenye thamani ya zaidi ya milioni 50 ikiwa njia ya kuongeza ushirikiano baina ya kampuni hiyo na wananchi.

Akipokea kwa niaba ya serikali Waziri wa Madini Doto Biteko alisema amefurahishwa na hatua ya kampuni hiyo ambayo imefanya utafiti wa madini ya kinywe ambayo yanatumika kutengeneza mabetri na sasa wapo katika hatua ya ujenzi wa mgodi hivyo kufikisha malengo ya serikali ya awamu ya tano kwa sekta ya madini kuchangia asilimia 10 ya pato la ndani ifikapo 2025.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ulanga Godfrey Mlinga alisema mbali na uwepo wa makampuni mbalimbali katika utafiti wa madini hayo jimboni la ulanga lakini amefurahishwa na hatua ya kampuni ya Mahenge Resources kwa kushirikisha wananchi kila hatua wakati wa utafiti na kudai kukamilika kwa mgodi huo utasaidia kuongeza ajira katika eneo hilo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Black Rock Mining ambayo ni kampuni mama ya Mahenge Resources John De Vries alisema baada ya kufanya utafiti wa madini hayo ya kinywe katika eneo la mahenge wamelidhishwa na ubora wa madini hayo kimataifa na wameshatumia dola za kimarekani milioni 23 katika hatua ya awali ya utafiti na sasa wapo katika hatua ya kulipa fidia wananchi ambao wapo eneo litakalogusa uwekezaji wa mgodi.