Kampuni ya Agrocom Tanzania imeendesha mafuzo kwa wafanyakazi wake, juu ya namna ya matumizi sahihi ya Trekta mpya na za kisasa za Kampuni ya Kubota kutoka nchini Japan, ambazo zitaanza kuuzwa na kampuni hiyo hapa nchini. Pichani ni Mkufunzi kutoka Kampuni ya Kubota, Kazunori Sasaki akitoa mafunzo hayo, yaliyofanyika kwenye Tawi la Agricom, Melela Mkoani Morogoro leo.
 Mmoja wa Mafundi wa Kampuni ya Kubota ya nchini Japan, Hiroshi Iwashita akiwaonyesha baadhi ya Wafakazi wa Kampuni ya Agricom namna Betri ya Trekta aina Kubota L 4508 inavyotakiwa kufungwa, wakati wa mafunzo maalum ya matumizi ya Trekta hizo, yaliyoandaliwa na Kampuni ya Agricom Tanzania.
 Muonekano wa Trekta mpya aina ya Kubota L 4508 za nchini Japan, zikiwa tayari kwa kazi mbalimbali za kilimo.
 Baadhi ya Mafundi na Wafanyakazi wa Kampuni ya Agricom Tanzania, wakiwa katika mafunzo ya vitendo.