Kamati ya Amani mkoa wa Mbeya wameiahidi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)kupeleka elimu ya kujikinga  na uhalifu  wanapotumia huduma za mawasiliano  kwa waumini  wao kama walivyoumbwa ili ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa ustawi  wa nchi yetu
 Viongozi hao

Wameyasema hayo  walipokuwa  semina  ya kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano  ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja  haingizwi  chaka  inayolenga  katika kuelimisha umma ya kujikinga.

 Wakichangia  katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi  za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda  wateja na kuahidi  kushiriki katika  kampeni  hiyo.

Viongozi hao wametoa wito  kwa taasisi  nyingine  kuiga mfano  wa TCRA katika  kuelimisha  umma kwani viongozi wa dini wanawafuasi wengi  na ushawishi  mkubwa  ktk  jamii  Kampeni  ya Sirububiki  Mjanja haingizwi  chaka  imeandaliwa  na Mamlaka ya Mawasiliano  kushirikiana na Jeshi  la polisi  kitengo cha uhalifu  mitandaoni  yenye lengo la kuelimisha  jamii jinsi ya kujikinga  ili wasirubuniwe wanapotumia  huduma za mawasiliano.

 Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania. Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali

Nae Mkuu wa Kanda ya Nyanda za  Juu Kusini wa TCRA Asajile John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.

Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana sana na teknolojia yake inabadilika kila siku .John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama  kwa ustawi wa nchi.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanatumia mawasiliano vibaya mkono wa sheria utawakuta.
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi akitoa maelezo kuhusiana na Kujikinga na Uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja katika Semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya
 Mkuu wa Nyanda za Kusini Asajile John akizungumza na Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya kuhusiana na Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ya Uhalifu katika Semina iliyofanyika jijini Hapa.
 Mmoja wa Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa Mbeya akisoma ujumbe ambao ametumiwa ambao uanaonyesha ni Uhalifu wa utumiaji huduma za mawasiliano.
Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Semina ya TCRA ya Kujikinga na Uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.