Jacqueline Mengi amesema amenyamaza kwa mambo mengi na kwa sasa anazuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wake.

Amesema anafukuzwa kuingia katika kaburi hilo pamoja na watoto wake na kutakiwa kuomba ruhusa ya kuingia katika kaburi hilo.

Jacqueline aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema hatakubali kuendelea kuonewa na watoto wake.

Aliandika ujumbe huo “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia Mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu, tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na baba wa watoto wangu!.. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya,” aliandika Jacqueline.