MREMBO kutoka tasnia ya Filamu nchini Irene Uwoya, amefunguka kuhusu uwezo alionao mwanae aitwae Krish wa kufanya shughuli za nyumbani ikiwemo wa kutandika kitanda huku akimpa ujira wa shilingi 5000.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Irene Uwoya, alisema kuwa mwanae kila anapotoka shule huwa amwomba afanye kazi ndogondogo na yeye humpa kiasi hicho cha pesa kama kifuta jasho.

“Mwanangu Krish amekuwa mkubwa kwa sasa anafanya baadhi ya kazi za nyumbani kama kuosha vyombo, kufagia na kutandika kitanda ili apate pesa, huwa namlipa shilingi 5,000 kwa wiki,”

“Namfundisha kuishi maisha tofauti tofauti lakini kwa upande mwingine inamsaidia kwa kiasi kikubwa kujuwa na kuweza kufanya kazi za nyumbani”alisema Irene Uwoya.