Msanii wa filamu na mchekeshaji, Idris Sultan ameanza mwaka 2020 kwa kusaini dili kubwa ya brand za nguo za Brands Outlet ambayo kwa sasa duka lake linapatikana Palm Village Shopping Mall Mikocheni Jijini Dar es Salaam ambapo dili hilo liliambatana na dili lingine la partnerships ya ghorofa kubwa nchini Tanzania la Palm Village Shopping Mall. Idris hakuweka wazi thamani ya dili hilo huku akidai kwamba ni moja kati ya dili zake kubwa kuwahi kuzifanya katika maisha yake ya sanaa. Muigizaji huyo amedai kupitia brand hiyo ya nguo ataachia bidhaa mbalimbali.

VIDEO: