Mchezaji wa Aston Villa ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, amethibitisha kuwa watu zaidi ya 10 kwenye familia yake, watakuwepo kwenye uwanja wa Wembley kutazama fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Man City.

Samatta ameweka wazi hilo kwenye mahojiano aliyofanya na The Gaurdian, ambapo amelieleza gazeti hilo pamoja na mtandao wao, kuwa ndugu zake hao watakuwa jukwaani.

'Zaidi ya wanafamilia/ndugu 10 wa Mbwana watakuwepo kwenye uwanja wa Wembley jijini London Uingereza, wakimtazama akicheza mechi ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Man City kesho Saa 1:30 Usiku', wameandika The Guardian.

Katika mahojiano hayo Samatta hajataja ni ndugu gani watakakuwepo London, kumtazama akiweka historia hiyo ya kucheza Wembley ambao ni uwanja wa taifa wa England.

Samatta amesajiliwa na Aston Villa kwenye dirisha dogo na tayari ameshafunga goli kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Premier League ambayo ilikuwa dhidi ya Bournamouth.