Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kushoto) akimsikiliza Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel alipokuwa akimuelezea namna inavyofanya kazi moja ya mashine za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), zilizotolewa na Taasisi ya Doris Mollel (DMF) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki. Taasisi hiyo hiyo imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 20 kwa hospitali ya Kisarawe ili viweze kutoa huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ikiwa pamoja na kuanzishwa rasmi wadi ya watoto Njiti kwa hospitali hiyo, ambapo hapo awali wazazi waliokuwa wakijifungua watoto njiti walikuwa wakipewa rufhaa ya kwenda Muhimbili au Mloganzila, ila kwa sasa watapata huduma hiyo hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akizungumza katika hafla ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 20, vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel (DMF) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki. hafla hiyo ilienda sambamba na kuanzishwa rasmi wadi ya watoto Njiti kwa hospitali hiyo, ambapo hapo awali wazazi waliokuwa wakijifungua watoto njiti walikuwa wakipewa rufhaa ya kwenda Muhimbili au Mloganzila, ila kwa sasa watapata huduma hiyo hospitalini hapo.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 20, vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel (DMF) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akumuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo sehemu ya vifaa hivyo.
Mama Getrude Mongela ambaye ni Mwanadiplomasia nguli na mpiganaji wa haki za wanawake aliyekua Mgeni wa heshima katika kafla hiyo akimkabidhi mmoja wa wakina mama waliojifungua watoto njiti, zawadi wakati waliopowatembelea kwenye wadi hiyo, hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.