Staa wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amepata umaarufu mkubwa si kwa usanii tu bali pia kwa jinsi anavyoishi maisha ya kifahari

Si magari, si nguo, si vipusa, si pesa, Mondi  hufanya kila awezalo kuhakikisha kwamba maisha anayoyaishi ni ya hadhi yake

Msanii huyo alijimwaya katika ukurasa wake wa  Intagram kuwakumbusha wasanii mahasimu kuwa yeye ndiye simba, hii ni baada ya kuchapisha video akicheza na mabunda ya noti kitandani

Ni dhahiri shahiri kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii ambaye anaishi maisha ya kifahari na ya kistarehe zaidi, si Tanzania tu bali pia kote Afrika Mashariki.


Mondi kamwe hakubali kuwa kuna msanii yeyote mwengine ayeweza kumshinda kwa urefu wa mkwanja na hivyo inakuwa desturi yake kuwakumbusha kwa namna yoyote kuwa yeye ndiye simba.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Instagramu, Mondi aliichapisha video akicheza na kujifurahisha na mabunda ya noti akiyarusharusha ya kujishaua kwayo huku ametayatandika kote kitandani.


Alijifanya kama anayehesabu hela hizo huku akilichukua bunda baada ya jingine na kurusha kando.

Inaaminika kuwa hii ilikuwanjia ya kuwaonyesha wasanii mahasimu kuwa kimo chake kifedha ni cha aina yake.


Ikumbukwe kuwa alipokuwa akiabiri ndege kusafiria Sierra Leone 2019, Mondi alichukua nafasi ya kumkumbusha Ali Kiba kuwa yeye ndiye jogoo.

Alikuwa akieleza kuhusu jinsi sanjari yake ilivyojaa, kuwa ana shoo kadhaa za kimataifa ambazo baadi yazo hawezi kuyakumbuka, hii yote ikionyesha uzito wa hela.