Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imesema uchunguzi wa sakata la manunuzi ya vifaa vya zimamoto na uokoaji yasiyozingatia sheria na taratibu za nchi ambao ulisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto Thobiasy Andengenye umekamilika kwa asilimia 99.9

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, ameviambia vyombo vya habari kuwa uchunguzi umebaini makosa mengi katika mkataba wa manunuzi hayo ambayo kwa pamoja yanatengeneza kosa la uhujumu uchumi.

READ More:HARUFU ya Asili ya Mwanamke ni Very Romantic Kuliko ya Kujipulizia Pafyumu..!!!!

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo TAKUKURU wanapeleka taarifa ya uchunguzi huo kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali tayari kwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote 17 wa sakata hilo