Mchezaji wa Yanga SC Bernard Morrison amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons FC Jeremia Juma wakati mpira ukiwa umesimama kwenye mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Timu ya Yanga SC imetozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kwa kosa la timu hiyo kushindwa kuwasilisha fomu ya wachezaji wao kwenye Pre match meeting ya mchezo Mechi namba 220- Yanga SC 0 vs Tanzania Prisons 0 uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.