Waziri wa Nchi Ofisi ya Aaziri Mkuu - Uwekezaji, Anjela Kairuki akisalimiana na Meneja Mwandamizi wa Wateja wa Serikali wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti alipotembelea Banda la CRDB, baada ya kufungua Kongamano la wawekezaji mkoani Songwe lililoandalia na Mkuu wa Mkoa huo, Brig. Jenerali Mstaafu, Nicodemus Mwangela kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kukuza na kuleta chachu ya maendeleo ya uwekezaji mkoani songwe. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Kanda Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka. 

Waziri Kairuki aliipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mdau mkubwa katika kuleta chachu ya maendeleo nchini kwakuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawawezesha wadau na sekta mbalimbali kwa kutoa mikopo ya uwekezaji. Aidha aliwataka wawekezaji Songwe na nchini kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na benki hiyo. Benki ya CRDB ni moja ya wadhamini katika kongamano hilo  linalofanyika kwa siku tatu ambalo lilitanguliwa na semina elekezi iliyoendeshwa na mkuu huyo wa mkoa Februari 15, 2020 na linatarajia kufikia kilele Februari 17, 2020 katika viwanja vya CCM mjini Vwawa.
Mkuu wa Mkoa huo, Brig. Jenerali Mstaafu, Nicodemus Mwangela akiwa katika banda la Benki ya CRDB alipopita kukagua na kupata maelezo mafupi kutoka kwa Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Denis Mwoleka pamoja na Meneja Mwandamizi wa Wateja wa Serikali wa Benki hiyo kutoka makao makuu, Nuru Kateti na kulia ni ndugu mathias mushi meneja mahusiano idara ya mikopo uwezeshaji wa biashara. Mkuu wa mkoa aliambatana na viongozi wengine wa serikali mkoa katika maadhimisho ya uwekezaji yaliyo fanyika mkoani songwe.
Meneja Mwandamizi wa Wateja wa Serikali wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti akizungumza katika kongamano hilo. Aidha aliwakaribisha wadau wa uwekezaji nchini kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na benki hiyo; “benki ya CRDB inatambua na kuthamini juhudi za serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa letu. Mwaka jana 2019, benki ilitoa jumla ya shilingi trilioni 3,4 kwaajili ya uwezeshaji katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa pamoja na biashara na uzalishaji viwandani, sekta ya kilimo, ujenzi, usafirishaji, nishati na madini, mafuta na gesi. Pia tunatoa mkopo wa uwezeshaji wa kufanyia bishara na uwekezaji, pia kutoa mafunzo ya utaalamu wa biashara kwa wafanya biashara ikiwa ni sehemu ya mkakati kuelimisha jamii juu ya namna bora za uendeshaji wa biashara.
Wateja mbalimbali wakipata huduma na maelekezo kutoka kwa maofisa wa benki walipotembelea banda la crdb benki katika viwanja vya ccm mkoani songwe katika kongamano la uwekezaji.