Katibu wa Itikadi na Uenezi ndugu Humphrey Polepole akimpongeza Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vicent Mashinji mara baada ya kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkutano uliofanyika katika ofisi ndogo za Chama Lumumba Jijini Dar es salaam. Februari 18, 2020.

AMETUA CCM! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk.Vicent Mashinji kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

DK.Mashinji aliyejiondoa Chadema Desemba mwaka 1919 amefikia uamuzi wa kujiunga CCM leo Februari 18, mwaka 2020 ambapo akitangaza uamuzi huo akiwa Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam akiwa amepokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

Akizungumza wakati akitangaza kujiunga na CCM ,Dk.Mashinji amesema kuwa ametafakari kwa kina hali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii ameona ni wakati muafaka kwake kujiunga na CCM ili ashiriki katika kuleta maendeleo ya Taifa lake.

Amefafanua kuwa akiwa Katibu Mkuu wa Chadema kwa nafasi hiyo alikuwa pia Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Demokrasinia kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kwamba fursa hiyo ilimfanya akawa Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Umoja wa vyama vya kidemokrasia Afrika pamoja na kuwa Mjumbe wa Umoja wa Vyama vya Demokrasia Duniani

"Sasa baada ya kukaa na kutafakari kwa kina na kuangalia jinsi ambavyo mwenendo mzima wa siasa,uchumi na shughuli za kijamii katika taifa letu, nikaona kwamba nadhan ni muda muafaka sana kuongeza kasi ya kuchochea maendeleo ya watu na vitu. 

"Katika kuangalia utayari kwamba akina nani wako tayari ,sisi tunaoamini katika mlengo wa kati kulia kuanzia mavazi ile itikadi pamoja na tunachokifanya, katika kukaa na kutakari nikaona Tanzania haiumbwi na malaika ,Tanzania inaumbwa na binadamu, na binadamu wanatofautiana uafadhali hivyo

"Lengo kubwa la nchi yetu ni maendeleo kwa hiyo fursa ya kukaa tunalumbana asubuhi mpaka jioni,hiyo inatuchelewesha , tunapochukua watu ambao ni wanataaluma halafu inakuwa kila siku ndani ya Chama ni malumbano,nje nalumbano sasa tutaendelea wakati gani ,kwa hiyo nikaona ni heri nije hapa Lumumba nizungumze na wenzangu nione kama ninaweza kupata fursa ya kutoa mchango wangu katika kujenga Taifa langu,"amesema Dk.Mashinji.

Ameongeza kuwa mimi yeye bado ni kijana anaweza kuwa hazina kwenye taifa lake na kama Rais anavyosisitiza maendeleo hayana Chama."Na ni kweli lazima tushirikiane pamoja na tuijenga nchi yetu, nimeona nije CCM na kama Mwenyekiti ataridhia basi anipe nafasi nijiunge na CCM kwani najua kama Mtanzania ninayo nafasi ya kushiriki kuleta maendeleo na kupata fursa zaidi ya kuchangia nchi yangu kupata maendeleo na hiki ndicho kitu kikubwa kwangu."