Wakati bado yupo nchini Marekani akifanya shughuli zake binafsi MwanaHipHop Roma Mkatoliki, ameweka rekodi mpya ya kushika namba 1 kati ya wasanii 10 wa HipHop  Afrika Mashariki wenye wafuasi wengi katika mtandao wa YouTube.

Akitoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya Instagram na Twitter, Roma Mkatoliki anaongoza kwa kuwa na wafuasi 265k.

Orodha ya wasanii wengine ambapo namba  2 imekwenda kwa Nyashinski 252k, Kenya 3. Darassa 240k, Tanzania   4. Khaligraph Jones 220k, Kenya  5. King Kaka 219k, Kenya  6. Nay Wa Mitego 180, Tanzania  7. Dogo Janja 161, Tanzania  8. Octopizzo 143k Kenya  9. Proffesor Jay 119k Tanzania  10. Young Killer 91k Tanzania.

Kwa upande wa Roma Mkatoliki Mwenyewe amesema "HipHop na Rap ni muziki unaopendwa sana na watu na una mashabiki wengi sana, sina uhakika  na hili,kwamba kwenye  "Digital Platforms" hatuna wafuasi wengi  ukilinganisha  na aina nyingine za muziki,  kwahiyo mimi kuwapata wafuasi  265K  na kuwa namba 1  Afrika Mashariki na Kati, haikuwa rahisi hata kidogo, hii ni baraka"