Baada ya Mtangazaji mwenye ushawishi wa kituo cha Times FM Ommary Rajabu Saleh Tambwe aka Lil Ommy kuaga rasmi kuwa hatoendelea kuwa mfanyakazi wa kituo hikch alichokifanyia kazi kwa muda mrefu akitokea VoT FM (Voice of Tabora FM) takribani miaka 10, tetesi zimekuwa nyingi.

Wengine wanadai nguvu ya pesa imemnyakua, na kuwa anaenda kujiunga na kituo cha redio cha Wasafi FM.

Ukirejea kauli zake kadhaa na mahojiano aliofanya kwenye kipindi cha Salama, alidai alishawahi kukutana na Marehemu Ruge na alikuwa akimuhitaji ila walikuwa kwenye mazungumzo.

Kikubwa alisisitiza ofa ni nyingi ila hawafiki kwenye makubaliano/muafaka na kupelekea abaki kwenye kituo mama anachofanyia kazi.

Lil Ommy ana deal nyingi sana. Pengine mshahara wa Times ulikuwa wa kawaida ila aliamua ajitengenezea himaya akiwa pale.

Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:

Je, ni kweli anaenda kujiunga na Wasafi FM?

Je, Clouds wanatimiza mazungumzo yaliyoanzishwa na Ruge?

Anaenda kujenga empire yake na kuwa mkubwa zaidi kama walivofanya Sky Walker, Sam Misago na MillarAyo?

Anaenda ku-deal na kipindi chake walichokuwa wameanza kukitengeneza na Raque?

Kuna kampuni kubwa imemtaka kumsimamia kwa ukubwa zaidi ndiyo maana kasepa na timu yake?

Tuache muda uzungumze na tuachane na "Tetesi", pesa anayopata/alizopata kutoka kwenye matangazo ni nzuri: Minutes Maid, TOTAL, Johar Rotana, Coca Cola, nk zinaweza kumfanyia kitu na siyo kwenda kuwa chini ya watu tena.

NB: Next week, J3, atawajuza nini anafanya na yupo wapi.

Tchao!