Mkongwe wa muziki hapa nchini Abdul Misambano, amefunguka na kusema wimbo wake wa Asu ulifanya watu wengi wapate wapenzi wapya na waliotengana kwenye mahusiano walirudiana.Akipiga stori na Big Chawa kwenye show ya PlanetBongo ya East Africa Radio, Abdul Misambano kipindi cha wimbo huo unatamba alipata umaarufu mkubwa na watu kupata wapenzi japokuwa haina video mpaka sasa.

"Asu ni nyimbo yangu ambayo watu wengi walipatia wapenzi wapya, watu wengi walirudiana na waliotengana kwenye mahusiano wakasamehana, kama nitafanya video ya wimbo huo halafu nikiambiwa nichague video queen awe Wema Sepetu na Hamisa Mobetto, basi atakuwa ni Wema Sepetu ndiye nitakayemchagua" amesema Abdul Misambano.

Pia msanii huyo amesema  nyimbo za sasa hivi haziwezi kudumu  kwa miaka miwili kwa sababu wasanii wanatoa nyimbo kila siku na wasanii wamekuwa wengi tofauti na zamani.