Msanii wa HipHop Young Dee amezua kihoja mitandaoni baada ya kuonekana amevaa  nguo aina ya kimono, vazi ambalo hupendelea kuvaliwa zaidi na wanawake.
 ike

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na Twitter, Young Dee ameshea picha hiyo kwa kupost akiwa amevalia vazi hilo kisha ameandika maneno yenye lugha ya kiingereza ambapo kwa kiswahili yanatafsirika kama,

"Pale msichana wako ambapo amekuibia nguo zako zote na ikiwa mida ya show, sijui itakuaje"

Baadhi ya maoni ya watu ambao wame-comment kwenye picha hiyo wameonekana kutoridhishwa kwa Young Dee kuvaa nguo hiyo huku wengi wao wakimkashifu na kumtukana kwa kufanya hivyo.