EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na Jacqueline Wolper, ambaye amefunguka kusema ataendelea kuishi maisha ya gharama na kula bata katika maisha yake yote kwa sababu anatafuta sana pesa.


Msanii huyo wa filamu amesema kuwa bora pesa zake azitumie kwenye bata, kuliko ikatokea siku amedondoka halafu watu kuanza kugombania pesa zake, ambazo amezitafuta mwenyewe.

"Siwezi kupunguza kwa sababu natafuta sana pesa, halafu mimi sitaki kuua watu kwa ajili ya pesa zangu kwa mfano nadondoka mtu anakuja kugombania pesa zangu ambazo nimezitafuta mwenyewe, sasa kwanini nisiitafute niiweke niifanyie mambo mengine mengine ya maana, napenda maisha mazuri nitakula bata na mtaendelea kuniona hivyo mpaka mwisho" ameeleza Jacqueline Wolper.

Pia Jacqueline Wolper ameongeza kusema sasa hivi amebadilika sana na hataki mambo ya mwaka 2019 yamtokee tena, na mchungaji wake amemwambia akitaka kubadilika basi aache mambo yote na mwaka huu atauona mpya kwake na vitu vipya