Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Dkt. Donald Kosanga, akiwa katika moja ya kivutio cha utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara.
Wanamuziki walio katika Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) wakijipiga picha wakati wa ziara hiyo.
Ziara ikiendelea.
Wanamuziki walio katika Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO)wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha bendera ya Taifa.
Na Dotto Mwaibale, Manyara.
WANAMUZI waliokatika Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii vilivyomo katika hifadhi hiyo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa Rais wa TAMUFO Dkt.Donald Kisanga alisema wametembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kuona vivutio mbalinbali vya utalii vilivyomo ili waweze kuvitangaza kipitia muziki.
"Tumefanya ziara hii ya kuona vivutio vilivyomo katika hifadhi hii ili tukirudi tuweze kuvitangaza kupitia muziki" alisema Dkt. Kisanga.
Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel akizungumzia ziara hiyo alisema imeshirikisha wanamuziki kutoka kada zote wanaounda umoja huo.
Alitaja wanamuziki hao kuwa ni bongo flava, muziki wa dansi, Rhumba, Injili na wa asili.
Baadhi ya wanamuziki waliokuwepo kwenye ziara hiyo amewataja kuwa ni Mzee Kingikii, Hamza Kalala, Emmanuel Mbasha, John Shaban, Emanuel Mabisa, Upendo Nkone, Agnes Mayagila, Babustar, Samatta Rajab, vikundi mbalimbali vya muziki wa asili na wengine.
Viongozi wa Tanzania Music Foundation (TAMUFO) walioongozana na wanamuziki hao kuwa ni Rais wa TAMUFO na Katibu Mkuu Stellah Joel na kuwa kila mwaka watakuwa wakitembelea hifadhi mbalimbali kwa lengo la kuzitangaza kupitia muziki.
Rais wa TAMUFO Dkt. Donald Kisanga ametumia nafasi hiyo kutoa raiametoa kwa watanzania kuanzia mtu mmoja mmoja familia na vikundi mbalimbali vya kijamii kujiwekea Utaratibu wa kutembelea hifadhi zetu za Taifa kama sehemu ya kuwa Wazalendo kama Rais wetu Dkt. John Magufuli anavyosisitiza kuwa na uzalendo kwa kila Mtanzania.