Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (kulia) akizungumza wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na Wakala wa Vipimo nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, iliyofanyika jijini Dodoma jana. Waziri Bashungwa amewaagiza Wakala wa Vipimo kuendelea kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kuwaelewa vizuri na hatimaye Tanzania ya viwanda iweze kutusukuma kufikia uchumi wa kati. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Suleman Sadiki na katikati ni Katibu wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Zainabu Mkamba.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Suleman Sadiki (katikati walioketi) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati yake wakati Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege (kushoto aliyesimama) alipokuwa akitoa wasilisho mbele ya wabunge kamati juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akitoa wasilisho mbele ya wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira pamoja na kuelezea mafanikio ya miaka minne ya serikali ya Awamu ya tano. katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Suleman Sadiki na kulia ni Katibu wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Zainabu Mkamba.
Baadhi ya wabunge wakichangia mada wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na Wakala wa Vipimo nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, iliyofanyika jijini Dodoma jana.
Baadhi ya wajumbe kutoka Wakala wa Vipimo na Wizara ya Viwanda na Biashara wakifuatilia majadiliano wakati wa semina.