Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akizungumza mara baada ya kutembelea vivutio vya Magofu ya Kale yaliyopo mji Mkongwe, Bagamoyo -Pwani huku akiwa ameongozana na wabunge wenzake wenye ulemavu ziara iliyokuwa imeratibiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV.

Chama cha Wabunge wenye ulemavu kimewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuendelea kusimamia vyema vivutio vya Mji Mkongwe na Kaole vilivyopo Bagamoyo huku kikiwataka wadau wa Utalii kutengeneza mazingira rafiki yatakayowawezesha watu wenye walemavu kufika kirahisi kutembelea hifadhi hizo.

Hayo yamezungumzwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa mara baada ya kutembelea katika vivutio hivyo huku akiwa ameongozana na wabunge wenzake wenye ulemavu ziara iliyokuwa imeratibiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Amesema kuwa ni vyema Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wa utalii wanaosimamia hifadhi za Taifa na vitutio vya asilia akiwemo TFS, TAWA na TANAPA ni vyema kutengeneza miundombinu rafiki itakayoweza kuwasaidia watu wenye ulemavu nao kutembelea hifadhi hasa katika upande mambo ya kale.

"Napenda nitoe pongezi zangu kwa Kamishna Mhifadhi Mkuu wa TFS Prof. Dos Santos Silayo na timu yake kwa ujumla kwa kuweza kuwa na vijana mahili wanaojua kutoa elimu sahihi kwa wageni wanaotembelea katika hifadhi zote wanazosomamia ila niwaombe kuendelee kusimamia vyema huku mkitengeneza mazingira rafiki ya miundombinu ili kutuwezesha tufike kwa wingi kutembelea mambo ya kale," amesema Naibu Waziri Ikupa.

Ameongeza kuwa kwa sasa serikali haipo nyuma kuendelea kutoa elimu kwa wamiliki wa hoteli, watoa huduma kwa jamii kuwapa kipaumbele walemavu ili nao waweze kujikwamua na wasonge mbele kimaendeleo kuliko kubaki wakiwa omba omba.

"Serikali ya Awamu ya Tano haipo nyuma katika kuwashika mkono walemavu ili waweze kusonga mbele kimaendeleo hivyo niwaombe wenzangu wenye ulemavu kuacha kulemaa na kubaki wakiwa omba omba bali wafanye kazi kwa bidii ili waweze kusonga mbele kujenga uchumi wa Taifa," Amesema Naibu Waziri Ikupa.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki Bi. Caroline Malundo akiwakaribisha wabunge wenye ulemavu mara baada ya kutembelea katika eneo la Mji Mkongwe, Bagamoyo ambapo kuna vivutio vya magofu ya kale. Wabunge hao walikuwa kwenye ziara iliyokuwa imeratibiwa na TFS. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa TFS.
Wabunge wenye Ulemavu wakipatiwa maelezo ya historia ya Mji Mkongwe mara baada ya kuwasili kujionea vivutio vya eneo hilo.
Katibu wa Chama cha Wabunge wenye Ulemavu Mhe. Amina Mollel akitoa machache.
Mbunge wa Ulyankulu, Tabora Mhe. John Kadutu (kulia) akizungumza neno mara baada ya kukaribishwa na na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel wakati wa ziara yao ya utalii mjini Bagamoyo - Pwani.
Wafanyakazi wa TFS wakifuatilia.
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wenye Ulemavu Mhe. Riziki Lulida ambaye ni mmoja ya mabalozi wa Utalii akitoa shukrani zake kwa TFS kwa namna ilivyoweza kuwapokea na kuwakarimu wakati wa ziara yao ya utalii mjini Bagamoyo - Pwani.


Muongoza watalii Bw. Cathbert akitoa maelezo kwa wabunge waliofika kutembelea vivutio vya mji mkongwe Bagamoyo - Pwani.
Muongoza watalii Bw. Cathbert akitoa maelezo juu ya vivutio vya mji mkongwe Bagamoyo - Pwani.
Moja ya kibao.
Boma ya Wajerumani iliyojengwa mwaka 1897 katika mji Mkongwe Bagamoyo - Pwani.
Boti zikisubiri mzigo kuelekea Zanzibar kutokea mji wa Bagamoyo - Pwani.
Wavuvi wakielekea kuvua samaki katika Bahari ya Hindi.
Shughuli za kuandaa chombo zikiendelea.
Wachuuzi wa vinyago wakionyesha biashara zao.
Mbunge wa Ulyankulu, Tabora Mhe. John Kadutu (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika eneo la Magofu ya Kale yaliyopo mji mkongwe, Bagamoyo
- Pwani.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misiti Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki Bi. Caroline Malundo akizungumza na wanahabari.

Kwa upande wake Meneja wa TFS Kanda ya Mashariki Bi. Caroline Malundo amewaomba Watanzania kujitokeza kutembelea vivutio vya misitu asili na mambo ya kale ili kuweza kujipatia elimu na historia ya kale ya mababu zetu.

Amesema kuwa katika jitihada za kukuza utalii na kukuza pato la Taifa, TFS kwasasa imeongezewa vivutio mbali na Misitu asilia pia imepewa dhamana ya kusimamia Magofu ya Kale yaliyopo mji Mkongwe na Kaole, Bagamoyo - Pwani, Michoro ya Miamba, Kolo- Kondoa, Magofu ya Tongoni - Tanga.

Aidha TFS imejipanga kusimamia na kuendeleza vyema vivutio vya mambo ya kale na kuweza kuvipa kipaumbele zaidi ili Watanzania wasiweze kupoteza historia ya mababu zetu.
Bango linaloelezea kwa ufupi mji wa Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Wageni kutoka mataifa mbali mbali wakipata maelezo mara baada ya kutembelea mji wa Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misiti Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki Bi. Caroline Malundo (kushoto) akizungumza na wageni aliwakuta eneo la Kaole Bagamoyo-Pwani.
Muongoza watalii akitoa maelezo kwa wageni.

Moja ya msikiti ambao ni kivutio katika mji wa Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Makaburi.
Moja ya kaburi lenye mnara refu kuliko yote.
Mbunge wa Ulyankulu, Tabora Mhe. John Kadutu akinawa maji ya baraka katika kisima kilichopo mji wa Kaole ambapo kisima hicho hutoa maji kwa mwaka mzima bila kukata. Inasemakana maji hayo huondoa mikosi na kuwapatia watu baraka.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel (mwenye kilemba) akinawa maji ya baraka.
Wabunge wenye ulemavu wakiongozwa na Naibu Waziri Stella Ikupa wakipita kujionea vivutio katika mji wa Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel akifanya sala katika makaburi ya Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Moja ya Bango lililopo  katika eneo la Bandari ya Zamani iliyopo Kaole, Bagamoyo - Pwani.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akiwa katika kaburi la Sharifu, kaburi hili hutumika katika matambiko mbali mbali ikiwemo kutoa mikosi.