MKURUGENZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akizungumza wakati wa kikao cha Mfuko huo na Waandishi wa Habari mkoani Tanga
Meneja wa Masoko na Huduma Kwa Wateja (NHIF) Hipoliti Lello akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa kupanua wigo wa wanachama wa NHIF wakati wa kikao hicho
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga Ally Mwakababu kushoto akisistiza jambo katikati ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray na anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Benard Konga.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga Ally Mwakababu kushoto akiwa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Benard Konga akisisitiza jambo kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Christopher Mapunda kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu.
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Arusha Isaya Shekifu.
Dinna Mlwilo wa NHIF Tanga akifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
Maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa kwenye kikao hicho.
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye kikao hicho katika aliyevaa suti ni Dege Masoli wa Nipashe.
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga Amina Omari akiuliza swali kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) Hassani Hashim akiuliza swali kwenye kikao hicho
Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando akiulizwa swali katika kikao hicho
Mwandishi wa Gazeti la Majira wilayani Korogwe Yusuph Mussa akizungumza wakati wa kikao hicho
MKURUGENZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Benard Konga amesema kwamba mfumo wa vifurushi vya bima ya afya hautakwenda kuua mfuko huo bali utakuwa ndio chanzo kingine cha mapato hatua itakayowasaidia kuboresha huduma zao kwa wanachama.
Konga aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Waandishi wa Habari mkoani Tanga kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo alisema kwamba vitakuwa na manufaa makubwa kwa watanzania.
Alisema kwamba mfumo wa bima ya Afya ni muhimu sana kwa watanzania kwa ajili ya kupata matibabu wakati wanapougua hivyo ni muhimu kuhakikisha wanajiunga na mpango wa vifurushi ambayo vitakuwa msaada mkubwa sana kwao na jamii zinazowazunguka.
Kauli hiyo ya Mkurugenzi huyo inatokana na swali aliloulizwa na Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga Mashaka Mhando ambaye alieleza kwamba mfumo huo wa vifurushi utakwenda kuua mfumo huo.
Akijibu swali hilo Mkurugenzi huyo aliwatoa hofu watanzania na kueleza kwamba uwepo wa mfumo huo wa vifurusi utakuwa chachu kubwa ndani ya mfuko huo kwa sababu unakwenda kuongeza chanzo kingine cha mapato na hivyo kusaidia kuboresha huduma wanazozitoa kwa wanachama wao.
“Ninaamini kwamba mfumo huo wa vifuriushi utaleta wanachama wengi wanakaoleta michango itakayowezesha mfuko kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kuwahudumia wanachama hao hivyo una faida kubwa sana “Alisema Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo alisema kwamba kuhusu watanzania kumudu gharama mfuko huo alieleza wameangalia mazingira halisi ya kipato cha mtanzania na kubaini wanaweza kumudu gharama hizo kutokana utafiti walioufanya.
“Lakini niulize kwamba wana habari hapa simu mnazomiliki hapa ukiangalia ni za bei juu sana na tunachangia masherehe tutoke huko tutambue kwamba uwekezaji kwenye afya zetu kwa manufaa yetu sisi wenyewe na Mwenyekitk wangu amekuwa akisema suala hilo sio siasa hivyo tuweke siasa pembeni tujiunge na mfuko huo”Alisema Mkurugenzi huyo.
Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Meneja wa Masoko na Huduma Kwa Wateja (NHIF) Hipoliti Lello alisema kwamba licha ya kuongeza magonjwa ya yasiyoambukiza na matatibu yake kuwa ya juu lakini bado wananchi wengi hawajapata mwamko wa kujiunga na Bima ya Afya.
“Akitolea mfano wastani wa matibabu ya mgonjwa mmoja wa Kansa kwa mwaka mmoja anatumia zaidi ya milioni 69 kwa ajili ya matibabu na kwa upande wa mgonjwa wa figo anatumia milioni 35 kwa mwaka huku mgonjwa wa moyo akitumia zaidi ya milioni 12.5 kwa mwaka kulingana na gharama hizo ifike wakati watanzania waone umuhimu wa kujiunga na bima ya Afya waweze kupata uhakika wa matibabu”Alisema
Alisema kuwa ili kujihakikisha huduma bora za matibabu ni muhimu watanzania wakaama na kujiunga na mfuko huo kwani kutokana na maboresho ya sekta ya afya kwa sasa matibabu lazima yatakuwa na gharama.
Awali akizungumza katika kikao hicho Mweka hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) Gift Kika aliushukuru mfuko kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wana habari kwani wanadhamana kubwa ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.