Dar24 kwa mara ya kwanza imefanya Exclusive Interview na baba mzazi wa Naseeb Abdul ”Diamond Platinumz”, Mzee Abdul ambapo amefunguka mambo mengi kuhusiana na maisha aliyokuwa akiishi na familia yake kabla hawajatengana na baada ya kutengana.

Mzee Abdul amefunguka sababu iliyopelekea kutengana na Bi Sandra wakati Diamond Platinumz akiwa kidato cha kwanza.

Lakini pia Mzee Abdul ameeleza kinachomkera sana kufuatia umaarufu na utajiri wa mtoto wake pamoja na maisha anayoishi mama yake kulinganisha na maisha yake ambayo yameonekana kuwa duni.

”Mtoto wake tajiri anauwezo lakini hakufanyii hivi wengi wanataka wanione mimi natembelea gari nakaa kwenye nyumba nzuri, wanione nina vitu vizuri vizuri tuu, na kitu ni chake katafuta yeye ndio mwenye uamuzi anaweza kusema leo baba nimfanyie hivi, ila mimi hata saivi akisema asinifanyie chochote kwangu ni sawa tu siwezi kuanza kupiga kelele sababu katafuta mwenyewe” amesema Mzee Abdul.

Aidha alipoulizwa kama amewahi kujutia kuiacha familia yake katika maisha duni hali ambayo ipo tofauti kwa sasa ambapo tunaona Diamond ni kijana mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka kufuatia kazi yake nzuri ya muziki iliyomlipa kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo amesema

”Sijawahi kujuta, bahati mbaya yule angekuwa tofauti hajapata,angerudi kwa babake, angekaa kwangu tungeishi kama kawaida, sijutii hili suala, Mungu alinipangia niwe nao katika kiwango kile” amesema Mzee Abdul.

Sikiliz kisa kizima katika link hapa chini.