Na Collin Ndanzi, globu ya jamii,
Mkali wa mchezo wa MMA (Mixed Martial Arts) Conor Anthony Mcgregor (32) ameandika historia mpya katika maisha yake baada ya ushindi dhidi ya mpinzani wake, Donald Cerrone (Cowboy) katika uwanja wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas.
Katika pambano hilo ilimchukua Mcgregor sekunde 40 tu kumtwanga mpinzani wake Donald katika raundi ya kwanza la mpambano huo na kushinda kwa TKO.
Mcgregor ameshinda pambano hilo ikiwa ni takribani mwaka tangu aingie ulingoni na Pambano lake la mwisho Mcgregor kushiriki ni kati yake na mhasimu wake Khabib Nurmegomedov ambalo, lilishuhudia Connor Mcgregor akipoteza mkanda wake wa ubingwa wa UFC 229 kwa mpinzani wake huyo katika pambano lililofanyika October 2018.
Lakini Mcgregor amefanikiwa kuwanyamazisha mashabiki na watu waliokuwa wakimsema katika mitandao ya kijamii baada ya kufanikiwa kupata ushidi huo mnono. Watu wengi walisema kuwa baada ya Mcgregor kupoteza pambano dhidi ya Khabib amekuwa akiishi maisha ya anasa na wengi kusema huenda hatapanda katika ulingo huu.
Bingwa wa UFC uzito wa kati Michael Bisbing ameweza kumwagigia sifa nyingi Conor Mcgregor baada ya ushindi huo. “ Hii inafumba midomo kwa wale waliokuwa wanasema kuwa Conor Mcgregor anafanya anasa”
Pambano linalomfwata Mcgregor tayari lipo katika mazungumzo na wadau wengi na mashabiki wa mchezo wa MMA ikiwa ni siku chcche baada ya Mcgregor kupata ushindi huo. Hivyo mashabiki wa mchezo huo wa ngumi wapo na shauku kubwa ya kuona kama Mcgregor atakuwa amerudi kwa ajili ya ushindi.