Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi Regna Chonjo akizungumza na wataalamu wa sekta mbalimbali waliokutana mkoani Morogoro katika kuboresha taarifa ya nchi kuhusu ubaguzi dhidi ya wanawake iliyo fanywa na wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
 Mkurugenzi Msaidizi Wanawake idara ya maendeleo ya jinsia akisisitiza jambo wakati wa kufunga kikao cha maandalizi ya taarifa ya nchi ya mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake.
 Wataalamu kutoka sekta tofautitofauti waliokutana mkoani morogoro kujadilina kuboresha taarifa ya nchi kuhusu ubaguzi dhidi ya wanawake.

Wataalamu kutoka sekta tofautitofauti waliokutana mkoani morogoro kujadilina kuboresha taarifa ya nchi kuhusu ubaguzi dhidi ya wanawake.


Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi Regna Chonjo amewataka wanawake nchini kutokata tamaa kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kutokana na kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo na kubainisha kutokata tamaa itasaidia kubadilisha fikra za wanawake wengi nchini kupinga vitendo hivyo.


Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga kikao cha maandalizi ya taarifa ya Tanzania ya mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake iliyofanywa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambapo akabainisha licha ya serikali kufanya mipango mingi ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vituo vya polisi kote nchini akatumia nafasi hiyo kuwasihi wanawake kote nchini kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapambana na vitendo hivyo sambamba na kutumia vyema nafasi wanazo patiwa ikiwemo maswala ya uongozi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake Wizara ya Afya idara kuu maendeleo ya jinsia Bi Mboni Mgaza akazungumzia namna walivyo jadili mikataba mbalimbali hasa inayohusu ubaguzi dhidi ya wanawake na utekelezaji wake ili kuiwasilisha umoja wa mataifa na kujadiliwa kwenye mkutano mkuu wa umoja wa mataifa unao tarajiwa kufanyika march mwaka huu na kubainisha utakua na majibu chanya kuhusu maswala ya ukatili hapa nchini.