Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini (TICTS), mwishoni mwa wiki walikusanyika kwa pamoja kufanya mazoezi ya kuimarisha afya zao, mazoezi yanayofanyika kila mwanzo wa mwaka kwa Wafanyakazi hao kufanya shughuli mbalimbali za michezo ili kuimarisha afya zao mahala pa kazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza hilo, Mkurugenzi wa Shirika na Maendeleo wa Kampuni hiyo, Donald Talawa amesema wafanyakazi hao wamekusanyika kwa pamoja kufanya shughuli hizo za michezo ili kuimarisha afya zao na kuleta tija wawapo kazini.
“Wafanyakazi wamefanya riadha ya KM 5 na 21, Mpira wa Miguu, kuvuta kamba na michezo mbalimbali, tunaamini hii italeta tija na ufanisi mahala pa kazi kwa kufanya hivi mara kwa mara”, amesema Talawa.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyakazi hao, Getrude Lamu amesema wamefanyakazi wamefurahi sana kufanya mazoezi katika michezo mbalimbali katika bonanza hilo, amesema wamehamasisha michezo hiyo mahali pa kazi kwa kufanya mazoezi mara kwa mara.
“Wafanyakazi wa TICTS katika bonanza la leo wamefika kwa wingi na wamefurahi sana kufanya bonanza hili, mwezi huu ni mwezi wa mazoezi, tunashughuru utawala wa Kampuni yetu kuleta kitu hiki kwa Wafanyakazi wetu”, amesema Getrude Lamu. Endelea kuangalia picha mbalimbali za michezo hiyo hapo chini.