NaChalila Kibuda,Globu ya Jamii Morogoro

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa vifaa vya Teknolojia ya Habari Mawasiliano (Tehama) na komputa 20 kwa shule za Sekondari Mzumbe pamoja na Kilakala zilizopo Mkoa wa Morogoro.

Vifaa hivyo wamefunga pamoja na mashine ya kuchapia karatasi , Internet pamoja na Komputa 10 kwa kila shule hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Komputa na Vifaa vya Tehama katika shule hizo Mwakilishi wa Katibu wa Tawala Mkoa wa Morogoro Afisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro Tullo Fundi amesema kuwa vifaa vilivyotolewa lazima vitunzwe na kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi kujua Tehama.

Amesema kuwa TCRA imetambua umuhimu wa Tehama na kuamua kutoa Komputa ambapo kwa Dunia ya sasa Tehama haipukiki.

Fundi amesema kuwa shule za sekondari Mzumbe na Kilakala zimepata vifaa hivyo kutokana na kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kitaifa hivyo juhudi zinahitajika kuendelea kufanya vizuri.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ,Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema amesema Mamlaka imekuwa na utaratibu wa kutoa vifaa vya Tehama kwa shule zinazofanya vizuri kitaifa kwa matokeo ya kidato cha nne ambapo kwa Kanda ya Mashariki shule hizo ziko tano.

Mhandisi Odiero amesema vifaa hivyo wamevitoa ni pamoja na matumizi salama ya mtandao."Ninaamini vifaa hivi mtatumia na kusaidia maendeleo ya shule kuendelea kufanya vizuri zaidi ikiwa ni kupata wataalam wa Tehama kutokana na kuwekewa msingi ya huduma hiyo"amesema Odiero .

Nae Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro Mildreda Selula amesema watatuza vifaa hivyo na kuongeza ufanisi katika somo la Komputa.

Amesema kuwa wataendelea kuongeza juhudi zaidi katika usimamizi wa kuendelea kufanya vizuri.Makamu Mkuu Shule ya Sekondari Mzumbe Edwin Matenga amesema TCRA imeongeza nguvu kwa kuwapa vifaa vya Tehama na kuandaa wataalam katika sekta hiyo.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkamkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ,Afisa Taaluma wa Mkoa Huo Tullo Fundi katika hafla uliofanyika Shule ya Sekondari Kilakala mkoani Morogoro katikati anayeshuhudia mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Wa Shule hiyo Mildreda Selula (katikati).
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilakala  Mkoani wa Morogoro , Mildreda Selula katika hafla uliofanyika Shule ya hiyo
 Picha ya Pamoja kati ya TCRA na Watendaji wa Mkoa wa Morogoro na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mzumbe

 Picha ya Pamoja Watendaji wa TCRA na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kilakala na Watendaji wa Mkoa wa Morogoro. 
 Afisa Mwandamizi wa Tehama wa TCRA Thuwayba Hussein akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kilakala Fatuma Jadi mara baada ya kujibu changamsha bongo wakati TCRA ilipokwenda kukabidhi Vifaa vya Tehama katika Shule hiyo.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkamkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ,Afisa Taaluma wa Mkoa Huo Tullo Fundi katika hafla uliofanyika Shule ya Sekondari Mzumbe katikati anayeshuhudia mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Wa Shule hiyo Edwin Matenga.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilakala wakiwa katika chumba cha Tehama