Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager, Pamela Kikuli(katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Sanaa ya uchoraji lijulikanalo kwa “Jiachie na Kili Canvas Competitions 2020” kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 1 mwaka huu Mkoani Kilimanjaro.Kulia ni Jaji Mkuu wa shindano hilo, Nathan Mpangala na Jaji msaidizi wa shindano hilo, Claud Chatanda.
Jaji Mkuu wa shindano la Sanaa ya uchoraji lijulikanalo kwa “Jiachie na Kili Canvas Competitions 2020”, kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 1 mwaka huu Mkoani Kilimanjaro, Nathan Mpangala, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager, Pamela Kikuli.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imezindua rasmi shindano la uchoraji nchi nzima linalojulikana kama “ Jiachie na Kili Canvas Competition 2020” na linalotarajiwa kufanyika Januari 22,2020 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema kuwa shindano hili litashirikisha wachoraji nchi nzima. Mshiriki atatakiwa kuja na kazi aliyochora kwenye Canvas (kitambaa kigumu cha kuchorea) kisichozidi sentimita 60 kwa sentimita 50. Mchoraji anapaswa kutumia vitambulishi vya bia ya Kilimanjaro Premium Lager kumuongoza katika uchoraji. Vitambulishi hivyo ni:
• Mlima Kilimanjaro
• Twiga
• Nyota Tano
• Michoro ya kiafrica iliyo kwenye lebo (pattern)
Kazi zitapitiwa na kuchunjwa na Majaji walioandaliwa na kupata washindi watano(5) ambao watapewa nafasi ya kuchora papo hapo (mubashara). Mshindi atapata nafasi ya kuchora mchoro maalum ambao utatumika kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon pamoja na pesa taslimu Shilingi milioni mbili(2,000 000/=).
Kikuli alisema, mashindano hayo yanafanyika kwajili ya kutoa fursa kwa wachoraji ili waonyeshe kazi zao kwa jamii, kuibua vipaji vipya pamoja na kuongeza muamko wa tasnia ya uchoraji nchini.
Shindano hili litafanyika ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mbio za Kilimanjaro Marathon 2020 ambayo hufanyika kila mwaka Mkoani Kilimanjaro.
Nae Jaji Mkuu wa Shindano hili, Nathan Mpangala, aliwaomba wachoraji wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ambayo kwanza itawatangaza, pili itawakutanisha na watu mbalimbali, itawajengea kujiamini na itawapatia kipato.
Kikuli alizitaja zawadi za washindi kuwa ni;