Jana nimemsikia presenta mmoja wa radio maarufu akidai kwamba "wasanii wa Nigeria wanaendelea sababu wana UMOJA, hawana ma-bifu". Hata wasanii wanaoheshimika bongo wamekua wakitoa hii hoja.

Je, ni kweli wasanii wa Nigeria wana UMOJA? (kwa kuangalia mfano wa Davido na Wizkid).Je, bifu zina faida au hasara gani?

Sasa hapa nime tafsiri makala kutoka mtandao wa Nigeria:

"Why The Ended Rivalry Between Wizkid And Davido Might Actually End Their Music Career"

Start/

Davido and Wiz.jpeg

Davido (a.k.a O.B.O) na Wizkid (a.k.a. Starboy) ni wasanii waliojizolea umaarufu mkubwa sana kwenye nyanja ya mziki nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla katika karne iliyopita. Wawili hawa walipata maarufu katika muongo mmoja, ambapo Wizkid alipata umaarufu mwaka 2011 na Davido 2012.

Bifu kati ya ma-star hawa wawili lilianza mwaka 2012, wakati Davido alipomtelekeza Wizkid Bar akiwa mlevi chakari na kuwambia wapambe wake wawapeleke wauza Bar nyumbani kwa Wizkid, ili alipe deni la bili la kiasi cha naira 500,000.

Wizkid akajibu mapigo kwa kukataa kushiriki kwenye album ya Davido ya O.B.O, akidai kwamba biti ya ngoma iliyoumwa kwake ilikuwa chini ya kiwango.

Msala hasa ulitokea pale Davido aliponyanyuka na kuondoka wakati Wizkid akipiga show kwenye tuzo za N.E.A huko New York. Mashabiki wa pande zote mbili walitetea pande zao na kutupiana vijembe. Matokeo ya hii drama ni kwamba ilichagiza msuguano na bifu, hivyo kuzima kabisa "AMANI" na maelewano waliyokuwepo baina ya ma-star hawa wawili. Bifu zina faida kwa wasanii kwenye tasnia ya sanaa? Jibu laweza kuwa ndiyo. Muulize Blackface, 2baba au Faze.

Mwaka 2013, kutokana na vita vya nani zaidi, Davido alipambana kufa na kupona ili awe juu ya Wizkid. Hii ilileta chachu kwa Davido kuachia singo kama “Gobe”, “One of a kind”, “Aye” na ngoma vairo (viral) “Skelewu”. Hii “Skelewu” iliambatana na video vairo za kucheza, ambazo zilisambaa Afrika nzima. Ghafla, Davido akawa amepanda na kufikia kiwango cha Wizkid.

Mwezi August 2014, Wizkid aliliamsha tena kwa ku-posti kwenye Insta yake alisema "TUMETUA NEW YORK CITY, TUNAFANYA SHOO KALI KWENYE VENYU KALI". Hii posti ilimlenga Davido, ambae alikuwa amefuta shoo yake New York City wiki chache kabla, kutokana na kukosa venyu. Mara baada ya hiyo posti, Davido nae akajibu kwa kusema "VUTA NUSU YA MASHABIKI WANGU KABLA HUJASEMA CHOCHOTE."

Hii iliwasha moto kwenye tasnia (huku tunaita "kiki"), ambapo kulitokea interviews, zilizopelekea vita kali ya maneno, kati ya mashabiki wa kambi hizi mbili, jambo ambalo lilichagiza ushabiki na kusaidia kupaisha umaarufu wa mziki wa ki-Nigeria ndani na nje ya nchi.

Mwaka 2015 Wizkid alirejesha ufalme wake kama msanii bora zaidi kwa kutoa album yenye mafanikio makubwa ikiitwa “Ayo”, pamoja na singo “Ojuelegba”, ambayo ilipelekea kufanyiwa remix na mzee mzima Drake na hata kusifiwa na mastar kama Alicia Keys na mumuwe Swizz-Beatz. Video ya rialiti star wa TV - Kylie Jenner akicheza "Ojuelegba" ilisambaa kwa kasi. Hii ilisaidia sana kumpa Wizkid umaarufu kimataifa, nje ya Nigeria na Afrika kwa jumla.

Mwaka 2016, Wizkid aliendeleza ufalme wake hasa kimataifa kwa kufanya kolabo na Drake na kutoa ngoma No. 1 kwenye chati za Billboard, “One Dance”. Davido, kwa upande wake, alikua bado akipambana kujulikana kimataifa, ingawa alifanya kolabo na mzee mzima Meek Mill na kusaini mkataba na kampuni ya Sony. E.P yake aliyoitoa chini ya mkataba na Sony haikua na mafanikio. Kumbuka, wakati huu Wizkid na Davido walikuwa wamesha sameheana na kuwa "MARAFIKI."

Peleka muda fasta mpaka 2017, ambapo drama mpya iliibuka kati ya Davido na Wizkid. Mwaka huo drama ilipoibuka, Davido alitoa singo kama “If”, “Fall” and “Fia”, huku Wizkid akita singo kama “Daddy Yo” na “Cime Closet”. Davido alipaa kwenye anga la kimataifa na singo yake ya "Fall" na kushinda tuzo ya MTV EMA, huku akiibeza tuzo ya AFRIMMA aliyoshinda hasimu wake Wizkid mwaka huo kwamba ni feki.

Wiki chache baadae, Wizid alifanya show iliyoisha tiketi (sold out) kwenye "The Royal Albert Hall na vile vile akashinda tuzo ya "MOBO mbele ya Cardi B, Jay-Z na Kendrick Lamar.

Kutokana na mafanikio ya 2017, mwaka uliofuata 2018 ukawaendea vizuri Davido na Wizkid bila kila mmoja wao kutumia nguvu nyingi sana. Walifanya shoo iliyojaza 02 Arena, yenye uwezo wa kuchukua watu 20,000 na kutoa singo kama “Soco”, ”Fake Love" na “Assurance”. Hata hivyo, Burnaboy bado aliwazima wote wawili na kukwea kileleni kama msanii bora wa 2018 alipokuja na albam yake ya "Outside" na singo vairo “Ye”.

Mwaka 2019 ukawaendea vibaya wote, Davido na Wizkid, ambapo hawakutoa singo yoyote kali na album zao za "A Good Time" (Davido) na "Soundman" (Wizkid) kutofanya vizuri. Wakati wao wakikwama, album ya “African Giant” ya Burnaboy ikatajwa kuwania tuzo za "Grammy". Hii ikampa chapuo Burnaboy (ukimlinganisha na Davido ba Wizkid), kama msaanii bora wa 2019.

Sasa swali kubwa la kujiuliza ni: Je, kile kilichoitwa "AMANI" kati ya Davido na Wizkid kinawaangusha kisanaa? Je, mafanikio ya Davido na Wizkid yamechagizwa na wawili hawa kuwa na bifu? Je, ufalme wa wawili hawa kwenye tasnia utanyakuliwa na Burnaboy na Naira-Marley katika kipindi kufupi kijacho?