Msanii wa muziki Gigy Money, amesema amekutana na wakati mgumu sana alipofanya mahojiano na mtangazaji Salama Jabir, hali iliyompelekea kumwaga machozi katikati ya mahojiano yao.


Kushoto pichani Gigy Money, kulia ni Salama Jabir

Gigy Money ni mmoja wa wasanii ambao watakuwepo kwenye show mpya ya SalamaNa, chini ya mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Salama Jabir  na itaruka kupitia East Africa TV kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku.

"Salama ni mtangazaji mkubwa na mtu mwenye hadhi ya kufanya mahojiano na sisi, huwa hacheki kirahisi, akiuliza swali yupo makini sana na akikupiga jicho huwa anamaanisha anachokuuliza, pia nililia kwa sababu alikuwa na maswali nyeti,yeye kina, uelewa na ukweli" ameeleza. 

"Uwepo wangu kwenye kipindi chake ina maanisha mimi ni staa kuliko wengine, na ugumu ambao niliokutana nao kwake sikuweza kudanganya, halafu nina hisia za haraka sana" ameongeza.