Na Collin Ndanzi, Globu ya Jamii

Wakati sakata la usajili juu ya beki wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly likiendelea barani ulaya, klabu ya PSG inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) imejiingiza katika mbio za kuwania saini ya Kalidou Koulibaly raia wa Senegal.

Kutokana na kiwango kizuri ambacho amekuwa akikionyesha Koulibaly kimeweza kuvutia vilabu kadhaa barani ulaya zikiwemo Manchester United, Manchester City, Liverpool, Juventus na klabu kadhaa barani ulaya.

 Manchester United wanatazamia kuwa mstari wa mbele wa kuwania saini ya Koulibaly ambapo kocha wa sasa wa kabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer akionekana kutaka kuimarisha kikosi hicho cha mashetani wekundu, lakini wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa matajiri hao wa jiji la Paris.

Koulibaly  ambae haonekani kufurahishwa na mwenendo wa klabu hiyo baada ya kocha Carlo Ancelotti kutimuliwa mapema mwezi Desemba, mwenendo wa matokeo ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 11 ikiwa pointi 27 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Juventus.\

Habari kutoka gazeti la La Gazzetta dello Sport via Foot Mercato ilitoa habari kuwa klabu ya PSG inaongoza njijia katika usajili wa beki huyo. Mwenyekiti wa klabu ya PSG Leonardo tayari ashafanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo na kutoa mkataba ambao utampatia mchezaji huyo pauni milioni kumi £10.2m kwa msimu, mkataba ambao ni mara dufu ya ule ambao klabu ya Manchester United imetoa kabla.

Miamba hiyo la jiji la Paris, ambao hivi karibuni wameonekana kuimarisha kikosi cha pia wanataka kuwekeza nguvu katika sekta ya ulinzi na Koulibaly anaonekana kuwa jibu sahihi kwao. 

PSG pia inajiandaa kuachia baadhi ya mastaa wao tegemezi Neymar na Mbappe ambao wamekuwa kivutio kikubwa kwa Barcelona, ambayo inataka kumrudisha Neymar katika klabu hiyo, na Real Madrid ambayo inaonejana kuvutiwa na kiwango cha Mbappe ambae amekuwa  kivutio kikubwa cha kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane.