Mwenyekiti wa timu ya Namungo akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya ubashiri sportpesa jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya ubashiri sportpesa na kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF) Wilfred kidao jijini Dar es Salaam.
Na Khadija Seif, Michuzi Tv.
TIMU ya Namungo fc waahidi kuonyesha maajabu kesho katika mchezo wao dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba fc.
Akizungumza hayo mara baada ya kutia saini makubaliano ya udhamini wa Kampuni ya ubashiri ya sportpesa baina ya timu ya Namungo Mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Zidadu amewashukuru sportpesa kwa udhamini huo na kuhaidi kufanya vizuri kutimiza malengo ya udhamini huo.
"Kupewa kwetu udhamini huu ni furaha na itakua chachu kwetu kufanya vizuri zaidi na kuhakikisha timu ya namungo inafika mbali zaidi ili Kampuni ya sportpesa wahamasike na kushawishika kuongeza donge nono zaidi ya hili".
Hata hivyo Zidadu ameeleza kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya simba na kuwahakikishia wapenzi wa namungo kuwa wamejipanga vizuri kuwakabili Simba.
"Kesho maajabu sio Simba kuifunga namungo bali maajabu yatakua namungo kuifunga Simba hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mtanange huo ".
Pia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya ubashiri ya sportpesa nchini Abbas Tarimba akiweka bayana udhamini huo uliogharimu shilingi za Kitanzania milioni 120.
"Tumeamua kudhamini timu ya namungo kutokana na weledi wake pamoja na bidii na wapo nafasi nzuri kwa sasa kwenye ligi kuu ambapo wapo nafasi ya tano na tumetoa udhamini wa milioni 120 na sio Mwisho tu tukiona wanafanya vizuri tutegemee dau litapanda zaidi,"