Mtoto wa Darasa la Pili nchini Kenya, ametumia kisu kujitahiri baada ya wazazi wake kushindwa kumudu kumlipia huduma hiyo inayogharimu Ksh. 1000 ambayo ni sawa na Tsh. 20,000.

Mvulana huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Itare amedai kufanya kitendo hicho takriban mwezi mmoja uliopita kutokana na hofu ya kutengwa na wenzake ambao tayari wamefanyiwa tohara.

Hali ya mtoto huyo kwa sasa sio nzuri na amekuwa akipata maumivu makali hasa wakati wa haja ndogo.

Watu wasiojulikana watokomea na vifaa vya NIDA
Hata hivyo wazazi wake wamelazimika kumrudisha nyumbani kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kisii baada ya kushindwa kumudu gharama za matibabu.