Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo akifungua moja ya Valvu katika kituo cha Kusukumia maji Salasala wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa uboreshaji huduma ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo amewapongeza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa juhudi kubwa wanayoifanya ya kusimamia miradi mikubwa ya mikubwa ya maji hadi kukamilika.
Mkumbo amesema, Dawasa wamekuwa wasimamizi wazuri wa miradi ya maji na wamefanikiwa kusimamia mradi huu wa ujenzi wa matanki na vituo vya kusukumia maji vilivyojengwa na Mkandarasi Jain kutoka India akisimamiwa na kampuni ya WAPCOS.
Akizungumza wakati ziara yake ya kutembelea miradi ya miradi, Mkumbo amesema malengo ya serikali ni kuona wananchi wanapata maji na kufikia asilimia 9tano kwa mijini na 8tano kwa vijijini.
Amesema, mradi huu mkubwa wa maji kwa mkoa wa Dar es salaam ulikua ni kwa ajili ya kuboresha na kuongeza huduma ya maji kwa maeneo yaliyokuwa na changamoto kubwa ya maji ambapo ulihusisha ujenzi wa matenki matano ya maji na vituo vya kusukumia maji (booster station).
"Kulikuwa na awamu mbili, tulianza na kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milion 300 hadi 500 kwa siku, na awamu ya pili ikiwa ni ujenzi wa matenki sambamba na vituo vya kusukumia maji kwenda katika matenki ya kuhifadhia maji yakiyojengwa maeneo tofauti,"amesema
“Mradi huu umekamilika, baadhi ya maeneo wananchi wameanza kupata maji kama vile maeneo ya Salasala na kilichobaki ni kwa viongozi kuja kuuzindua, kazi kubwa imefanywa na Dawasa kuhakikisha wanasimamia na kukamilika ili wananchi wapate huduma ya maji,”amesema
“Dhumuni kubwa la kufanya maboresho ni katika kuhakikisha maeneo yaliyokuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji au yaliyokuwa hayana maji yanaanza kupata huduma hii muhimu,”
Mkumbo ameeleza kuwa, kwa sasa kazi kubwa iliyobaki ni kuanza usambazaji wa maji kwa wananchi na tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Bilioni 77 kutoka mkopo wa Benki ya Dunia na utapita kwenye maeneo 20 kuanzia Dar es salaam hadi Bagamoyo.
Aidha, ametembelea maeneo yote yaliyohusisha Ujenzi wa matenki na vituo vya kusukumia maji katika maeneo ya Bunju, Wazo, Mabwepande, Salasala, Changanyikeni
Mbali na hilo, Mkumbo ameeleza kuwa serikali pia imepeleka Bilioni 117 Katika Wilaya 86 katika mikoa 17 na Kila wilaya imepata billion 1.36 na wamekabidhiwa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) ili kuboresha huduma ya maji vijijini kwa kujenga vityuo vipya na kufufua vya zamani ili kufikia malengo ya serikali ifikapo Desemba 2020 na amewaomba watendaji wa serikali kuhakikisha malengo yanatimia.
Pia, Serikali imepeleka Biloni 25 Wizara ya Afya kwa ajili ya hospitali na bilioni 7 kwenye Wizara ya Elimu ili kuboresha usafi wa mazingira ikiwemo kujenga vyoo vipya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo akiwasha kitufe cha kuruhusu maji katika kituo cha Kusukumia maji cha Salasala wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa uboreshaji huduma ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati ziara yake ya kutembelea mradi wa uboreshaji huduma ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati ziara yake ya kutembelea mradi wa uboreshaji huduma ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na moja ya wananchi waliounganishiwa huduma ya maji katika kata ya Salasala.