Msanii legend wa music wa bongofleva Mr Nice ameshangazwa na msanii Harmonize kuchukua vionjo wa wimbo wake kin'gasti Kwenye wimbo "Hainistui" bila kuniomba wala makubaliano.

Wakati Mr Nice akihojiwa amefunguka unajua kuchukua vionjo au beat au mistari ya msanii mwingine kwa kumuomba au kuingia makubaliano naye si jambo mbaya ni jambo zuri maana unakubali kazi ya mwenzako na hata wasanii wakubwa wa Marekani wanafanya hivyo kuliko hata sisi lakini wanafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za haki mimiliki ila huku bongo baadhi ya wasanii hawazingatii hili sasa ukitumia kazi ya mwenzako bila ridhaa yake huo ni wizi.

Ameongezea pia, namtaka Harmonize asirudie huo upuuzi tena nimemsamehe akirudia tena sitamuonea huruma nitamchukulia hatua za kisheria.

Hivi karibuni pia Harmonize alichukua beat na vionjo vya msanii Steve simple the boy bila ridhaa yake pamoja na msanii mwingine kutoka Kenya ikapelekea kutokea mzozo miongoni mwao.