Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,akitia saini kwa kutumia kifaa maalum,ikiwa ni kuridhia Makubaliano ya Sekta ya Nishati yaliyokubaliwa katika Mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wapili kulia) akichangia mada katika Mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki wakati wa majadiliano ya sekta ya Nishati kwa nchi wanachama
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kushoto) na Watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Nishati katika nchi za Afrika Mashariki unaofanyika kwa njia ya mtandao,ambapo hapa nchini ulifanyika Jijini Dodoma.

Na Zuena Msuya, Dodoma.
 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesaini makubaliano ya Sekta ya Nishati ya mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Waziri ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

Mkutano huo umefanyika Januari 14, 2019, ambapo kila nchi huufanya nchini kwake, hapa nchini mkutano huo umefanyika jijini Dodoma kwa kushirikisha Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati, Mashirika pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo.

Majadiliano ya Mkutano huo huendeshwa kwa njia ya mtandao (Video Conference) kwa kuwakutanisha Mawaziri wa sekta husika kutoka nchi zote wanachama.

Mkutano huo hujadili taarifa mbalimbali iliyowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu wa Wizara husika katika sekta hiyo zinayohusu miradi mbalimbali ya maendeleo ya Sekta ya Nishati katika nchi wanachama.

Taarifa hiyo ya Makatibu Wakuu, iliyowasilishwa kwa Mawaziri hayo imezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Umeme, Nishati Jadidifu, Mafuta pamoja Gesi.

Baada ya majadiliano hayo, Mawaziri wote wa Sekta ya Nishati wa nchi wanachama wa wameridhia na kusaini makubaliano ya kisekta, kwa lengo la utekelezaji.

Mawaziri walioshiriki mkutano huo ni kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda pamoja na Burundi.