Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WATALII zaidi ya 600 wamewasili nchini kutokea katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kutembelea vivutio vya Utalii.
Watalii hao wamewasili leo asubuhi na meli ya Azamara Club Cruise wakitokea katika Visiwa vya Sychells na takribani watalii 160 wameweza kushuka kwenye meli hiyo na kwenda katika vivutio vya utalii.
Baadhi ya watalii wameonesha kufurahishwa na mazingira ya Dar es Salaam, Tamaduni hususani nyimbo za kiasili na ukarimu wa watanzania.
Moja ya watalii hao kutokea nchini Japan, Minori Warabisako ameeleza kuwa hii ni mara ya kwanza kuja nchini Tanzania na amekuwa anatamani sana katika maisha yake kufika katika nchi za kiafrika na kwa mara hii amefika, amependa sana mazingira.
Minori amesema, mbali na kufika Tanzania pia atatembelea baadhi ya maeneo ya Vivutio vilivyopo na cha zaidi anaamini siku nyingine atakuja tena nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) John Sendwa amesema Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakishirikiana na Mamlaka ya Bandari TPA wameweza kuboresha miundo mbinu ya Gati namba tano ili meli kubwa kuweza kutia nanga.
“Zaidi ya watalii 160 wameshuka, wanaelekea sehemu mbalimbali, wengine wakielekea Masai Mara Kenya wapo wataokwenda Bagamoyo na wataotembelea hapa hapa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa lengo la serikali ni kuliweka kuwa mojawapo yaJiji la Kitalii,”
Sendwa amesema, wanapokuja watalii wengi kama hawa, mamlaka inapata mapato na serikali pia lengo la TTB ni kufikia watalii milioni 2 kwa mwaka.
Amesema, watalii hao wataondoka leo usiku na kuelekea Zanzibar na kisha wataenda hadi Maputo nchini Msumbiji na hii ni fursa zaidi ya zaidi ya kujitangza hasa baada ya serikali kuboresha gati kwa ajili ya kutoa huduma za kitalii.
“Watalii hawa wametoka nchi mbalimbali, na wameanzia America wametembea katika nchini za Suez Canal, visiwa vya Sychells hadi kufika hapa nchini na kuja kwako ni kuongeza kwa pato la Taifa kwa kutembelea vivutio,”
Meli hiyo imetia nanga leo na wataondoka usiku kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na utalii wao wa meli katika nchi mbalimbali duniani.
Bodi ya utalii inazidi kutumia nafasi wanazopata kuutangaza utalii wa ndani na Vivutio vya utalii nchini na kujenga ushirikiano na mawakala wa utalii duniani.
Baadhi ya watalii wakishuka kutoka katika Meli ya Amazara Club Cruise kwa ajili ya kwenda kutembelea maeneo ya Utalii ya ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na nje ya Dar es Salaam. Meli hiyo imetia nanga leo Katika Gati namba 5 ya Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) leo Jijini Dar es Salaam.
Moja ya watalii hao kutokea nchini Japan, Minori Warabisako ameeleza kuwa hii ni mara ya kwanza kuja nchini Tanzania na amekuwa anatamani sana katika maisha yake kufika katika nchi za kiafrika na kwa mara hii amefika, amependa sana mazingira na tamaduni za Afrika.
Kaimu Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) John Sendwa akizungumzia ujio wa meli ya watalii Azamara Club Cruise wakitokea katika Visiwa vya Sychells na takribani watalii 160 wameweza kushuka kwenye meli hiyo na kwenda katika vivutio vya utalii.