Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele amechangia shilingi milioni 13 kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Ndembezi kinachojengwa katika Mtaa wa Butengwa na zahanati ya Ngokolo.


Akizungumza katika kikao chake na Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi leo Jumapili Januari 5,2020, Mhe. Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) amesema katika awamu ya kwanza alitoa shilingi milioni tano na sasa anatoa shilingi milioni 6 kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwasogezea karibu wananchi huduma za afya.



“Ujenzi wa kituo cha afya Ndembezi ulianza kwa nguvu za wananchi,nilichangia shilingi milioni 5 na sasa naongeza tena shilingi milioni 6 hivyo kufanya mchango kuwa milioni 11 kwenye ujenzi wa zanahati hii mpaka sasa na nimeomba serikalini shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huu. Naamini pindi ujenzi utakapokamilika kituo kitawasaidia wananchi wa Ndembezi lakini pia wananchi wa kata za jirani”,alieleza Masele.


Akiwa katika kata ya Ngokolo,Masele pia ameahidi kuchangia shilingi Milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa zanahati ya Ngokolo ili kuwasogezea huduma za afya wananchi hivyo kufanya jumla ya mchango wake katika ujenzi wa kituo cha afya Ndembezi na zanahati ya Ngokolo kuwa shilingi milioni 13 mpaka sasa.

“Nitaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kutatua changamoto za wananchi hususani katika sekta ya elimu,afya,barabara,maji na umeme kwani tunachohitaji ni wananchi wapate maendeleo",alisema Masele.

Mhe. Masele leo Jumapili Januari 5,2020 amehitimisha ziara yake iliyoanza Desemba 27,2019 kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzungumza na wajumbe wa kamati za siasa CCM ngazi ya matawi na kata 17 za jimbo la Shinyanga Mjini.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi leo Jumapili Januari 5,2020 wakati akihitimisha ziara yake Jimboni aliyoanza Desemba 27,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Katibu wa CCM kata ya Ndembezi Pendo Sawa akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini, Amri Migeyo akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao na Mbunge Stephen Masele.
Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi wakipiga picha ya kumbukumbu na Mbunge wao Stephen Masele.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog